Ministry of Water

Singida Water Supply and Environmental Sanitation Authority

SUWASA KUBORESHA HUDUMA YA MAJI IKUNGI


Wataalam kutoka Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Singida (SUWASA) wakiwa Ikungi kwa ajili ya kufanya makabidhiano ya kazi ya maboresho katika Mradi wa Uboreshaji wa huduma ya maji katika Miji Midogo.

Makabidhiano hayo yamehusisha Wataalam wa SUWASA Fundi Sanifu Mkami Magesa, Msimamizi wa Kanda ya Ikungi James Malima na _Local_ Fundi Simon Maghembe.

Katika mji wa Ikungi Mradi huu una thamani ya shilingi milioni 30 ambapo fedha hii inatolewa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Mfuko wa Maji wa Taifa ambayo itajumuisha kazi za ununuzi wa mabomba na viungio, uchimbaji wa mitaro, ujenzi wa chemba, ubadilishaji wa mabomba yenye kipenyo kidogo, uwekaji wa alama za njia za mabomba (markerpost) pamoja na ukarabati wa tanki moja la Muungano lenye uvujaji.

Maboresho yanatarajiwa kufanyika pia katika maeneo yote ya miji midogo kama Ikungi, Puma, Iguguno, Sepuka na Irisya ambayo yanayohudumiwa na SUWASA, ili kuimarisha utoaji wa huduma.