SUWASA YASHIRIKI ZIARA YA WAZIRI MKUU MHE. MWIGULU NCHEMBA (MB) SINGIDA
Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Singida (SUWASA) imeshiriki katika Ziara ya Waziri Mkuu Mhe. Mwigulu Nchemba (Mb) Singida iliyofanyika tarehe 21 Novemba katika maeneo ya Manyoni, Ikungi na Singida Manispaa.
Ziara hiyo iliyoanzia Wilaya ya Manyoni na kukamilika Manispaa ya Singida ilihusisha ukaguzi wa miradi ya maendeleo na kuzungumza na wananchi.
Baada ya Ukaguzi wa miradi, Mhe. Mwigulu amefanya Mkutano maaluum na Viongozi wa Taasisi mbalimbali za mkoa pamoja na Watumishi wa Umma na baadae kukamilisha ziara hiyo katika mkutano wa hadhara na Wananchi katika viwanja vya Bombadia.
Amewaelekeza watumishi kutekeleza majukumu yao kwa kufanya kazi kwa bidii na kuepuka uvivu na uzembe. Amesema katika awamu hii atahakikisha watumishi wasiotimiza majukumu yao kwa uzembe wanachukuliwa hatua
Aidha amewataka watumishi kuepuka kushiriki vitendo vya uharibifu wa Mali za umma inayotokana na tofauti za kisiasa kwani kufanya hivo kunarudisha nyuma maendeleo ya Taifa letu
Akizungumza na Wananchi amewataka kuilinda nchi ya Tanzania na kuepuka vishawishi na kusikiliza maneno ya watu wenye nia mbaya ya kuharibu amani ya nchi.
Mwigulu amemshukuru Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania. Dkt Samia Suluhu Hassan kwa Kumwamini na kumteua katika nafasi hiyo, hali kadhalika viongozi wa Mkoa wa Singida na wananchi kwa kumpigia kura.