Mamlaka ya
Majisafi na Usafi wa Mazingira Singida (SUWASA) imepokea Wakaguzi kutoka
Ofisi ya Rais Tume ya Utumishi wa Umma ambao wamefika katika ofisi za
SUWASA kwa ajili ya ukaguzi wa kiutendaji katika maeneo mbalimbali ya
kiutumishi.
Wakaguzi hao ambao wameongozwa na Mkaguzi Kiongozi
Bi. Sheila Dachi wameeleza kuwa, huu ni Ukaguzi wa kawaida wa Mwaka
2024/2025 ambapo lengo ni kuhakikisha sheria za kiutumishi zinazingatiwa
katika utendaji.