Wizara Ya Maji

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Singida

SUWASA KUBORESHA HUDUMA YA MAJI MJI MPYA WA SATELITE WILAYA YA IKUNGI


Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Singida (SUWASA) inaendelea na jukumu la kuboresha huduma ya maji kwa wananchi ambapo imeongeza mtandao wa maji katika eneo la Mjimpya unaojulikana kama Satelite town katika wilaya ya Ikungi.

Upanuzi huu una thamani ya shilingi milioni 25.33 ambao unahusisha ununuzi wa mabomba yenye kipenyo cha 2' kwa umbali wa mita 2000, ununuzi wa viungio, ujenzi wa chemba za vizuizi pamoja na uwekaji wa markerpost kwa ajili ya kuonesha alama za mabomba.