Wataalam
kutoka Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Singida (SUWASA) wakiwa
Ikungi kwa ajili ya kufanya makabidhiano ya kazi ya maboresho katika
Mradi wa Uboreshaji wa huduma ya maji katika Miji Midogo.
Makabidhiano
hayo yamehusisha Wataalam wa SUWASA Fundi Sanifu Mkami Magesa,
Msimamizi wa Kanda ya Ikungi James Malima na _Local_ Fundi Simon
Maghembe.
Katika mji wa Ikungi Mradi huu una thamani ya shilingi
milioni 30 ambapo fedha hii inatolewa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania kupitia Mfuko wa Maji wa Taifa ambayo itajumuisha kazi za
ununuzi wa mabomba na viungio, uchimbaji wa mitaro, ujenzi wa chemba,
ubadilishaji wa mabomba yenye kipenyo kidogo, uwekaji wa alama za njia
za mabomba (markerpost) pamoja na ukarabati wa tanki moja la Muungano
lenye uvujaji.
Maboresho yanatarajiwa kufanyika pia katika maeneo
yote ya miji midogo kama Ikungi, Puma, Iguguno, Sepuka na Irisya ambayo
yanayohudumiwa na SUWASA, ili kuimarisha utoaji wa huduma.