Wizara Ya Maji

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Singida

SUWASA IMETOA ELIMU YA USOMAJI NA UTUNZAJI WA MITA ZA MAJI


Watumishi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Singida (SUWASA) wametoa elimu ya usomaji na utunzaji wa mita za maji.

Elimu hiyo ya nyumba kwa nyumba imetolewa kwa wakazi wa eneo la Utemini na Sabasaba ambapo watumiaji wa huduma ya maji, wameelekezwa namna ya kuhakiki usomaji wa mita za maji, ili kuepuka bili zisizoendana na matumizi pamoja na ushiriki katika utunzaji wa mita za maji, kwa kutoa taarifa za mita mbovu Uvujaji na uharibifu wowote wa mita unaojitokeza.

Watumiaji wa maji wamesisitizwa pia kushiriki katika kuhakikisha usalama wa mita za maji kama kuzieekea vizuizi ili kuepuka uharibifu kama kugongwa na madhara ya aina hiyo.

SUWASA kwa kushirikiana na Jeshi la polisi Singida inaendelea na uchunguzi kubaini waharifu wanaojihusisha na wizi wa miundombinu ya maji.

Elimu hiyo yenye lengo la kuepusha upotevu wa maji, kuondoa bili bambikizi na kuhakikisha usalama wa mita, inaendelea kutolewa katika maeneo Mengine ya Manispaa ya Singida.